epl

GUAARDIOLA ATAJA KILICHOWABEBA MBELE YA PSG

admin May 5, 2021 5:47 am

 


PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City amesema kuwa walipambana kwa pamoja jambo ambalo liliwafanya wao kutinga hatua ya fainali ya UEFA Champions League.

Ushindi wa mabao 2-0 mbele ya PSG katika nusu fainali ya pili imewafanya watinge hatua ya fainali kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-1.

Ni Riyad Mahrez alitupia mabao yote mawili dakika ya 11 na 63, Uwanja wa Etihad na Angel Di Maria wa PSG alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 69.

Kutangulia kwa City katika fainali kunawafanya  wasubiri mshindi wa mchezo kati ya Chelsea na Real Madrid utakaochezwa darajani leo majira ya saa 4:00 usiku.

Guardiola amesema:”Tulipambana kwa pamoja na kujituma, hili nina amini kwamba ni neno ambalo ninaweza kusema, kutinga kwetu hatua ya fainali ni jambo la furaha,” .


HAPA NDIPO AMBAPO YANGA INAKWAMA, WACHEZAJI WAKE PAMOJA NA MAKUNDI CAF YAONGEZA IDADI YA WACHEZAJI WA AKIBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply