Simba SC

ISHU YA VIINGILIO VYA SIMBA NA YANGA WAHUNI WAMEMCHEZEA HAJI MANARA NAMNA

admin May 5, 2021 10:47 am


OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kuna wahuni ambao wanasambaza clip ambazo zinataja viingilio vya mchezo huo kuwa ni 5,000 jambo ambalo sio kweli na lilisababisha apigiwe simu na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi Tanzania.

Simba ina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Mei 8, Uwanja wa Mkapa.

Manara amesema:-“Jana na juzi kuna clip inatembea sijui inataja viingilio kwamba viingilio ni 3,000, sijui 5,000 nikapigiwa simu na watu wa Bodi ya Ligi, TFF wakiniambia kwamba vile sio viingilio.

“Ile clip ni ya mwezi wa tisa kuelekea kwenye mechi yetu dhidi ya Gwambina sasa kwa kuwa iliangukia Jumamosi basi wahuni wakaamua kuitumia.

“Viingilio ni 7,000 mzunguko, 15,000 VIP C, 20,000 VIP B, 30,000 VIP A. Hakuna viingilio vya elfu tatu sijui hii ni mechi kubwa,” amesema.


JOSE MOURINHO SASA NI MALI YA AS ROMA YANGA: DAKIKA 90 ZITAAMUA NANI ATAANDIKA HISTORIA MPYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply