Yanga SC

YANGA: DAKIKA 90 ZITAAMUA NANI ATAANDIKA HISTORIA MPYA

admin May 5, 2021 10:47 am


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa ni dakika 90 ambazo zitaamua nani ataandika historia kwenye mechi ya Mei 8, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo umezidi kupanda joto kwa sasa ambapo timu zote zimekuwa zikipiga hesabu ya kupata pointi tatu katika mchezo huo muhimu.

Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 27 inakutana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 25.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa mashabiki na wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi uwanjani.

“Dakika 90 zitaamua kati ya sisi na wao nani anakwenda kutengeneza historia nyingine katika soka la bara la Afrika, tunakutana na watani zetu wa jadi Jumamosi hii na watani zetu.

“Mashabiki na Wanachama tunaomba wajitokeze kwa wingi, mashabiki wa Yanga na wapenzi wa Yanga njooni,” amesema. 

ISHU YA VIINGILIO VYA SIMBA NA YANGA WAHUNI WAMEMCHEZEA HAJI MANARA NAMNA GWAMBINA FC YAKOMAA NA KUBAKI LIGI KUU BARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply