Ligi Kuu

GWAMBINA FC YAKOMAA NA KUBAKI LIGI KUU BARA

admin May 5, 2021 11:47 am


 BADRU Mohamed, Kocha Mkuu wa Gwambina FC amesema kuwa watapambana kufanya vizuri kwenye mechi zao za ligi zilizobaki kwa mzunguko wa pili.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 27 imekusanya pointi 30 ipo nafasi ya 12 katika msimamo.

Mchezo wake uliopita ikiwa Uwanja wa Gwambina Complex iliyeyusha pointi tatu jumla kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC.

Badru amesema:”Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa hizi mechi ambazo zimebaki, bado nafasi ipo na mechi zimebaki ambapo tukifanya vizuri katika mechi hizi nafasi yetu itakuwa kubwa kubaki.

“Hakuna hesabu nyingine ambayo tunafikiria kwa sasa zaidi ni kuona kwamba tunapata pointi tatu, mashabiki wazidi kutupa sapoti,” amesema.

Ni Mwadui FC kwenye msimamo ipo nafasi ya 18 baada ya kucheza mechi 28 imekusanya pointi 19 ipo kwenye mstari wa kushuka daraja na msimu huu kuna timu nne zitashuka jumlajumla na mbili zitacheza play offs.

YANGA: DAKIKA 90 ZITAAMUA NANI ATAANDIKA HISTORIA MPYA MAAMUZI YATOLEWE MAPEMA, LALA SALAMA INA MAMBO MENGI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply