Home Yanga SC SIMBA YATAJA WACHEZAJI HATARI WA YANGA, SAIDO, KISINDA NDANI

SIMBA YATAJA WACHEZAJI HATARI WA YANGA, SAIDO, KISINDA NDANI


 KUELEKEA mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya Simba dhidi ya Yanga, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amewachambua wachezaji wa wapinzani wao hao huku akiweka wazi kuwa Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Manara amesema kuwa Tuisila Kisinda na Saido Ntibazonkiza ndiyo wachezaji anaowafikiria zaidi wanaweza kuwasumbua katika mchezo wa leo, Mei 8 kwa upande wa Yanga.

 Simba watakuwa wenyeji wa Yanga katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, mchezo wa mzunguko wa kwanza timu hizo zilipokutana matokeo yalimalizika kwa sare ya bao 1-1.


Manara alisema kuwa licha ya watu kuiona Yanga haina wachezaji wazuri lakini anamuona mchezaji kama Feisal Salum kuwa ni mchezaji mzuri huku akiwataja Saido Ntibazonkiza na Tuisila Kisinda kuwa ni wazuri pia ambao wataweza kuwasumbua katika mchezo wa leo.

 

“Yanga inaonekana kama ina wachezaji wa kawaida lakini siyo kweli, kuna Feisal Salum ni mchezaji mzuri ambaye siku zote nampenda na kama nikiambiwa nimpe usajili aje Simba basi angekuwa wa kwanza kusajiliwa na anaweza kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Simba.

 

“Saido ni mchezaji mzuri lakini bahati mbaya umri umemtupa mkono hana spidi sana, Tuisila Kisinda ni mchezaji ambaye ana spidi kubwa, lakini namuona zaidi kwenye riadha kuliko uchezaji mpira, ukiwa Simba huwezi kukimbia kimbia tu hovyo.

 

“Lakini kwa mbio zake anaweza kutusumbua, hao ndiyo wachezaji kidogo ambao nawafikiria kwa upande wa Yanga watakaoweza kutusumbua,” alisema Manara.


SOMA NA HII  HARUNA NIYONZIMA KUAGWA LEO KWA MKAPA