epl

ARGUERO AOMBA MSAMAHA KUKOSA PENALTI

admin May 10, 2021 6:47 am


 SERGIO Kun Arguero, mshambuliaji wa Manchester City ameomba msamaha kwa kupiga penalti mbovu iliyowafanya wakose pointi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England mbele ya Chelsea.

Juzi wakati City wakichapwa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea walishindwa kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu England kwa sababu walikuwa wanahitaji ushindi.

Pia jana walikwama kuutwaa ubingwa huo baada ya Manchester United kushinda mbele ya Aston Villa hivyo bado City wanakazi ya kusaka ushindi kwenye mechi zao zilizobaki.

Nyota huyo amesema:”Napenda kuomba msamaha kwa wachezaji wenzagu, viongozi pamoja na mashabiki wa soka kutokana na kukosa penalti ile.

“Yalikuwa ni maamuzi mabaya sana na napenda kuwahakikishia kuwa lawama zote zinanihusu mimi,”.

Kocha Mkuu wa City, Pep Guardiola amesema kuwa alimuambia nyota huyo awe makini hivyo hawezi kujua ni jambo gani ambalo lilimkuta.

CAVAN KUPEWA MKATABA MNONO UNITED VIDEO:KUHUSU KUYEYUKA KWA KARIAKOO DABI, SIMBA WATOA TAMKO,

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply