Yanga SC

JEMBE HILI LA KAZI YANGA KAMILI KUUNGANA NA WENZAKE

admin May 17, 2021 4:47 am


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mapinduzi Balama anatarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake hivi karibuni ikiwa ni program maalumu ambayo amepewa.

Nyota huyo aliumia enka Juni, 2020 na kwa sasa anaendelea na matibabu ili kurejea kwenye ubora wake.

Msimu huu hajacheza mchezo hata mmoja wa mashindano ndani ya ardhi ya Bongo kwa sababu ya kutibu enka.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kwa sasa tayari ameshapona  na anatembea bila usaidizi wa  magongo.

“Kuhusu Balama kwa sasa anaendelea vizuri na amepona kwa kuwa anatembea bila ya usaidizi wa magongo. Anatarajiwa kuungana na wachezaji wenzake ikiwa ni program maalumu ambayo amepewa,” .

Chanzo: Championi.


YANGA KUIFUATA JKT TANZANIA KWA TAHADHARI LEO DAVID LUIZ ANASEPA MAZIMA ARSENAL

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply