Azam FC

AZAM FC : TUTAZIDI KUPAMBANIA JAMBO LETU

admin May 22, 2021 5:47 am


 NAHODHA wa kikosi cha Azam FC, Agrey Morris amesema kuwa bado wana kazi ya kufanya kwa ajili ya kutimiza malengo yao ndani ya Ligi Kuu Bara.

Azam FC ipo ndani ya tatu bora ikiwa inapambania kutimiza lengo la kutwaa taji la Ligi Kuu Bara ambalo lipo mikononi mwa Simba.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 60 baada ya kucheza jumla ya mechi 30, Yanga nafasi ya pili na pointi 61 imecheza mechi 29 na Simba namba moja imecheza mechi 25.

Nahodha huyo mzawa amesema:”Tunajua kwamba tuna jambo ambalo tunapaswa kutimiza, tutapambana katika mechi zetu ambazo zimebaki ili kupata matokeo chanya.

“Ushindani ni mkubwa na kila mchezaji anajua hilo jambo ambalo linatufanya tuzidi kupambana muda wote,” .

NIDHAMU INAHITAJIKA KWA SIMBA KUIKABILI KAIZER CHIEFS KWA MKAPA IHEFU YAKOMALIA KUBAKI NDANI YA LIGI KUU BARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply