Simba SC

HIVI NDIVYO GOMES WA SIMBA ANAVYOFIKIRIA KUHUSU YANGA

admin May 24, 2021 9:47 am


 HASIRA za Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes kwa sasa zipo katika kubeba makombe mawili ya ndani ambayo anashindania sambamba na watani zao wa jadi, Yanga.

 

Gomes amepania kumaliza msimu huu kwa kutetea mataji yao waliyoyatwaa msimu uliopita ambayo ni Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam.

 

Tayari ndani ya Ligi Kuu Bara, Simba ndiyo vinara wakiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 25.


Mbio zao za kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika zilikwama Mei 22 baada ya kutolewa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-3 ambayo Simba ilifunga.

 

 Gomes amesema: â€œKikubwa ni kuangalia namna ya kutetea mataji yetu msimu huu, haitakuwa rahisi kwetu kuona tunayapoteza na kwenda sehemu nyingine.

 

“Tutapambana kwa nguvu zote kutetea mataji yetu kwani malengo yetu ni kuona kwamba tunabeba mataji yote ambayo tutashiriki kwa sasa,”.


Msimu huu ikitokea Simba ikabeba tena mataji hayo, itakuwa ni msimu wa nne mfululizo Yanga inakosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam.


BEACH SOCCER NI WAKATI WA KUFIKIA MAFANIKIO SASA ISHU YA USAJILI YANGA WAMPA RUNGU NABI, WENGINE KUONGEZEWA MIKATABA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply