Azam FC

AZAM FC YAWAPA TANO WACHEZAJI WAKE KUITWA STARS

admin May 30, 2021 2:48 pm


UONGOZI wa Azam FC umewapa pongezi nyota wake watano kwa kutajwa kwenye orodha ya wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kikosi cha Stars kilitangazwa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen Mei 28.

Kinatarajiwa kuingia kambini Juni 5 mwaka huu ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi.

Wachezaji wa Azam FC ambao wamejumuishwa kwenye kikosi ni pamoja na Mudhathir Yahya, Salum Abubakar, Bryson Raphael, Ayoub Lyanga na Idd Seleman, ‘Nado’.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wachezaji hao wanapaswa pongezi kwa kujumuishwa kwenye kikosi hicho na wanapaswa kutimiza majukumu kwa ukamilifu.

NYOTA WATATU SIMBA WAWANIA TUZO MUKOKO WA YANGA ANASAKWA NA VIGOGO AFRIKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply