Home Tetesi za usajili EXCLUSIVE: MKUDE, AJIBU RASMI KUTUA YANGA MSIMU UJAO WA LIGI

EXCLUSIVE: MKUDE, AJIBU RASMI KUTUA YANGA MSIMU UJAO WA LIGI


Imeisha hiyo.., Ndivyo unavyoweza kusema mara baada ya wachezaji waandamizi wawili ndani ya kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Simba SC, Jonas Mkude na Ibrahim Ajib kusaini mikataba ya awali kujiunga na mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania, Yanga SC.

Taarifa za kuaminika kutoka kwa watu wakaribu na wachezaji wao, zinasema kuwa nyota hao kwa nyakati tofauti wameshamalizana na Yanga, na kinachosubiriwa tu ni msimu huu kuisha na kutambulishwa rasmi kwenye himaya ya GSM..

Mtoa taarifa wetu, amesema kuwa Ajib alimalizana na Yanga mapema zaidi kabla hata ya mechi ya kwanza ya robo fainal ya Klabu Bingwa, dhidi ya Kazier Chiefs nchini Afrika Kusini.

Inadaiwa kuwa Ajib ambaye hii itakuwa mara yake ya pili kujiunga na Yanga akitokea Simba , ameshasaini mkataba wa miaka miwili, na kuchukua kishika ‘uchumba’ cha milioni arobaini na tano.

Ajib amefikia hatua hiyo,mara baada ya kuona hapati nafasi ya kucheza ndani ya Simba, huku karibu makocha wote waliopita msimbazi pamoja na Gomes kutoridhiswa na aina yake ya uchezaji.

Aliyekuwa kocha wa Simba, Mbelgiji Sven Vandebroken aliwahi kunukuliwa mazoezini akimkaripia Ajib kuwa hafai hata kuvaa jezi ya Simba achilia mbali kuwa mchezaji wa timu hiyo.

Hali kama hiyo, pia imejitokeza kwa Gomes ambapo inasemekana mara kadhaa amekuwa akikosoa kiwango cha Ajib.

Ajib ambaye ni kipenzi cha mashabiki na viongozi wa Simba SC, amekuwa kwenye kiwango kibovu kupita kawaida toka ajiunge na Simba SC akitokea Yanga SC misimu miwili iliyopita.

Itakumbukwa akiwa Yanga, Ajib alikuwa ni nahodha na mchezaji wa kutegemewa , ambapo mpaka anamaliza mkataba wake na Yanga, alikuwa na ofa ya kwenda kuichezea TP Mazembe ya DR ongo kabla ya kuibukia mitaa ya msimbazi ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili.

Kwa upande wa Jonas Mkude, mto taarifa wetu amesema kuwa kiungo huyo mkongwe nchini amekamilisha hatua zote muhimu za kujiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.

SOMA NA HII  WAKATI WAKIJIANDAA NA SIMBA...NABI AIBUA MAPYA YANGA...BALAMA MAPINDUZI , ADEYUN WAHUSIKA...

Mkude ambaye ni mmoja ya wachezaji wakongwe ndani ya Simba , ataondoka mwishoni mwa msimu huu na kuhitimisha misimu kumi na moja ya kuwa na Simba.

Taarifa zinasema , Mkude amekubali kujiunga na Yanga, kwa sharti la kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza huku maslahi yake ya kimkataba yakihakikshiwa kuwa mazuri zaidi ya Simba.

Hivi karibuni, Mkude amekuwa katika hali ya mzozo wa kinidham na klabu yake, ambapo inasemekana tabia yake ya kuchelewa kurepoti kambini imekuwa ni kero kwa makocha wake na viongozi kwa ujumla.

Kwa kuwasajili wachezaji hao, Yanga itakuwa imelamba dume kwani uwezo binafsi na kutaka kuwaonyesha Simba SC kuwa walikosea kuwaacha vitawafanya wacheze kwa bidii zaidi msimu ujao.

Hata hivyo, Yanga itanufaika na uzoefu wao kwenye mashindano ya kimataifa, kwani mwakani kuna uwezekazno mkubwa wa timu yao kushiriki Klabu Bingwa Afrika.