Home Tetesi za usajili MTAMBO WA MABAO WA DODOMA JIJI WAWEKWA RADA NA YANGA

MTAMBO WA MABAO WA DODOMA JIJI WAWEKWA RADA NA YANGA


 IMEELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Dodoma Jiji, Seif Karihe yupo kwenye hesabu za Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi ili aweze kujiunga nao kwa ajili ya msimu ujao.

Habari zimeeleza kuwa kwa sasa Yanga ambayo ipo Mtwara kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC inamfuatilia kwa ukaribu mshambuliaji huyo.

Karihe amekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi cha Dodoma Jiji kinachonolewa na Kocha Mkuu, Mbwana Makata amefanikiwa kutupia mabao  7 akiwa amecheza jumla ya mechi 19 katika.

Dodoma Jiji imecheza jumla ya mechi 28 na kufunga mabao 26 na pointi zake ni 38 ikiwa nafasi ya 7.

Mtu wa karibu wa Karihe amesema kuwa Yanga imekuwa ikimfuatilia nyota huyo ili kuona kama anaweza kuwa chaguo la Nabi ambaye kwa sasa namtumia Yacouba Songne kwenye nafasi ya ushambuliaji.

SOMA NA HII  RONALDO KUJIUNGA NA WARABU KWA DAU LA TRILIONI 1...