Home news TIMU KIBA vs TIMU SAMATTA ZATOSHANA NGUVU

TIMU KIBA vs TIMU SAMATTA ZATOSHANA NGUVU


 UBAO wa Uwanja wa Samora leo Mei 21 baada ya dakika 90 kukamilika umesoma Team Kiba 1-1 Timu Samatta na kufanya timu zote kutoshana nguvu.

Mchezo huu ni maalumu kwa ajili ya hisani ya kurejesha kwa jamii ambao unafanywa na msanii wa Bongo Fleva, Ally Kiba na nyota wa mpira Mbwana Samatta kwa kushirikiana na wachezaji pamoja na wasanii wote bila kuwasahau wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakiunga mkono jitihada hizo.


Mradi huo umepewa jina unaitwa SamaKiba Foundaution, Nifuate ambapo mwaka uliopita ilikuwa ni Dar es Salaam.

Fedha ambazo huwa zinapatikana katika kiingilio huelekezwa kwa wenye mahitaji maalumu ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii na msimu huu ni wa kwanza kufanyika nje ya Dar es Salaam.

Ni Thabit Tishan dakika ya 14 alipachika bao la kuongoza kwa Timu Kiba baada ya kutengewa pasi na Rashid Juma na liliwekwa usawa na Badi Banca dakika ya 22.

Banca, mwili jumba alitumia makosa ya mabeki wa Timu Kiba kusawazisha bao hilo dakika ya 22 kwa pasi ya Agustin Alphonce.


SOMA NA HII  UANAAMBIWA KWA HAYA ANAYOPITIA MAYELE HUKO YANGA...MPAKA KAZE MWENYEWE ANASHANGAA...