News

MANJI NDANI YA BONGO

admin June 2, 2021 8:47 am


IMEELEZWA kuwa mfanyabiashara maarufu nchini ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amewasili nchini Tanzania Jumanne, Juni Mosi, 2021 jioni baada ya kukaa nje ya nchi kwa miaka kadhaa sasa.

 

Manji alikuwa akitajwa kuwa wakati wowote atarejea nchi amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


Taarifa zinaeleza kuwa alihojiwa kwa muda kadhaa na maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuhusu uhalali wake wa kuingia nchini.

 

Imeelezwa kuwa baada ya kutoa maelezo yake, aliachiwa baada ya maofisa hao kujiridhisha kuwa Manji ni Mtanzania na anayo haki na uhalali wa kuingia nchini Tanzania.

VIDEO:KUMBE CARLINHOS HAKUWA NA FURAHA YANGA, ALIGOMA KULA VIDEO: AJIBU ANUKIA KUTUA YANGA, GOMES AJIPA MECHI TANO KUTWAA UBINGWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply