Helbert Lukindo Namungo
Michezo Bongo

Helbert Lukindo Aitisisha Simba: Baada ya Mabao 3 Mfululizo, Namungo Kutoa Kipigo?

Vardo October 31, 2026 12:40 pm

Kasi ya mshambuliaji wa Namungo FC, Helbert Lukindo, inazidi kupamba moto katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, huku akiweka wazi nia yake ya kuandika rekodi mpya atakapokabiliana na vinara wa ligi hiyo, Simba SC.

Lukindo amekuwa kwenye kiwango bora baada ya kufunga mabao matatu katika michezo mitatu mfululizo (dakika 270), akiongoza jahazi la Namungo kupata pointi tisa muhimu zilizowapandisha hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 15.

Nyota huyo wa zamani wa Mbao FC, KenGold, na Tanzania Prisons alianza msururu wake wa mabao kwa kuifunga TRA United (1-0), kisha akafunga dhidi ya Coastal Union (2-1), kabla ya kuingia kwenye nyavu tena dhidi ya Polisi Tanzania (1-0). Kasi hii inamfanya afikishe mabao lima msimu hii, akiwa nyuma ya kinara wa ufungaji, Anuari Jabir wa Polisi Tanzania mwenye mabao saba.

Mbio za Kuisoma Simba SC

Baada ya mafanikio hayo ya mechi tatu zilizopita, miamba hiyo ya Ruangwa inajiandaa kushuka uwanjani Novemba 2, 2026, kucheza ugenini dhidi ya Simba SC—timu pekee kwenye ligi ambayo haijapoteza mchezo wowote hadi sasa, ikiwa imefunga mabao 20 na kuruhusu manne pekee.

Akizungumzia siri ya mafanikio yake na mchezo unaofuata, Lukindo alisema:

“Nashukuru mwanzo si mbaya, japokuwa inahitaji kuendelea kupambana kutokana na ugumu wa ligi na vita kali ya namba. Nimeaminiwa na benchi la ufundi, lazima nifanye kazi yangu. Kinachonirudisha nyuma mara kwa mara ni majeraha, lakini uwezo upo na nia ya kuipigania Namungo ni kubwa.”

“Tuko Tayari Kuwasimamisha Wababe”

Kuhusu mchezo wao unaofuata dhidi ya vinara wa ligi Simba SC, winga huyo machachari ametamba kuwa hawajali ukubwa au rekodi ya mpinzani wao.

“Mpira ni mchezo wa wazi. Tunajua Simba ni timu kubwa na hawajapoteza mechi hadi sasa, ila lolote linawezekana. Mkakati wetu ni kushinda kila mechi inayofuata, na huenda tukawa wa kwanza kuwasimamisha wababe hao wenye ukuta mgumu,” alisema Lukindo kwa kujiamini.

Huku Namungo ikisaka kujiweka pazuri zaidi kwenye msimamo na Lukindo akisaka viatu vya ufungaji bora, pambano hili linatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Makocha 6 Ligi Kuu Bara Wanaotembea Kwenye Kamba Nyembamba