JKT Tanzania vs Azam FC: Vita ya Pointi 3 Ligi Kuu Bara Leo
Mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara unatarajiwa kuwa na ushindani mkali pale JKT Tanzania itakapowakaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam, kuanzia saa 12:30 jioni.
Mchanganuo wa Msimamo wa Ligi Kuu Bara Azam FC kwa sasa inashikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi tisa (imeshinda 6, sare 2, imepoteza 1). Kwa upande wa JKT Tanzania, wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi 17 baada ya michezo 10 (imeshinda 5, sare 2, imepoteza 3). Ushindi kwa JKT Tanzania unaweza kubadilisha mwelekeo wa msimamo na kuwafanya wabadilishane nafasi kulingana na idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Nyota wa Kuchungwa na Takwimu zao Mabeki wa JKT Tanzania wana kibarua kizito cha kuwazuia washambuliaji hatari wa Azam FC:
-
Abdul Suleiman: Mwenye mabao 4 msimu huu.
-
Feisal Salum ‘Fei Toto’: Mwenye mabao 3 (alimaliza msimu uliopita nafasi ya pili kwa ufungaji bora akiwa na mabao 15).
-
Idd Selemani ‘Nado’: Mwenye mabao 2.
Kwa upande wa JKT Tanzania, safu ya ulinzi ya Azam FC inapaswa kumchunga sana Paul Peter, ambaye tayari ana mabao 2 msimu huu baada ya kufanya vizuri msimu uliopita kwa kufunga mabao 9.
Kumbukumbu ya Mechi Zilizopita (Head-to-Head) Msimu uliopita JKT Tanzania iliambulia pointi moja pekee dhidi ya Azam FC baada ya kutoka sare ya 1-1 mnamo Oktoba 1, 2025, kabla ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 Aprili 17, 2026.
Kocha na Wachezaji Wanasemaje?
-
Florent Ibenge (Kocha wa Azam FC): “JKT Tanzania ni miongoni mwa timu zenye ushindani mkubwa. Tunatarajia mchezo mgumu wenye chalenji nzuri, na kupishana kwa nafasi moja kunatupa chachu ya kupambana zaidi.”
-
Lusajo Mwaikenda (Nahodha wa Azam FC): “Kupata alama trois Meja Jenerali Isamuhyo siyo kazi rahisi, lakini ushindani wa JKT Tanzania unatupa nguvu ya kujituma zaidi.”
-
Ahmad Ally (Kocha wa JKT Tanzania): “Haitakuwa mechi rahisi, lakini maandalizi yamekamilika na tupo tayari kwa mapambano.”
-
Jafary Maneno (Mchezaji wa JKT Tanzania): “Benchi la ufundi limetutayarisha vyema. Tutapambana kuyafanyia kazi maelekezo yote ili kupata matokeo.”
Mtanange Mwingine Leo: Coastal Union vs Dodoma Jiji
Mbali na mchezo huo, Coastal Union watakuwa nyumbani kukabiliana na Dodoma Jiji saa 3:00 usiku. Msimu uliopita kila timu ilishinda mechi yake ya nyumbani (Dodoma Jiji 2-0 Coastal Union na Coastal Union 3-1 Dodoma Jiji).
Ushindi kwa Dodoma Jiji utawafikisha pointi 18, wakati Coastal Union (pointi 13) ikishinda inaweza kuziruka Singida Black Stars (pointi 14) na Namungo FC (pointi 15).
-
Vincent Mashami (Kocha wa Dodoma Jiji): “Siyo mchezo mwepesi, lakini tumejiandaa vyema kwa ushindani.”
-
Fikiri Elias (Kocha wa Coastal Union): “Kila mechi kwetu ni kama fainali, tumejipanga kupata pointi zote tatu nyumbani.”