Tetesi za usajili

BEKI WA AS VITA KUJIUNGA NA YANGA, MENEJA AELEZA WALIPOFIKIA

admin June 3, 2021 8:47 am


 BEKI wa kikosi cha AS Vita Djuma Shaban amekubali kujiunga na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Beki huyo raia wa Congo anatajwa kumalizana na mabosi wa Yanga ambao wapo kwenye mchakato wa maboresho wa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.

Ikiwa mambo yatakuwa hivyo basi Julai Djuma atatangazwa kujiunga na kikosi hicho akiwa ni mchezaji huru.

Nyota huyo amesema:”Nimeambiwa kwamba Yanga wanahitaji huduma yangu, mimi sina tatizo ikiwa kutakuwa na makubaliano mazuri nitajiunga na kufanya nao kazi. Suala hilo nimeliacha mkononi mwa uongozi,” .

Kwa mujibu wa meneja wa Djuma Faustino Mukandila amesema kuwa wapo kwenye mazungumzo na mabosi hao ambao wameonyesha nia ya kumpata beki huyo.

“Yanga wameonyesha nia ya kuhitaji huduma ya beki wetu hivyo kwa sasa tupo kwenye mazungumzo na ambapo tumefikia sio pabaya kila kitu kikiwa sawa tutaweka wazi,” amesema.

Beki huyo pia alikuwa anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na timu yake ili kumuongezea mkataba kwa kuwa bado wanahitaji saini yake.


JOHN BOCCO ANALIAMSHA DUDE KILA BAADA YA DAKIKA 56 VIDEO: IBRAHIM AJIBU ASAINI YANGA MIAKA MIWILI, ACHOTA MAMILIONI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply