Azam FC

DUBE, LWANDAMINA WASEPA NA TUZO MEI

admin June 7, 2021 1:48 pm


 NYOTA wa kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Mei.

Mshambuliaji huyo ni kinara wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa na jumla ya mabao 14 kibindoni kwa sasa msimu wa 2020/21.

Dube ametwaa tuzo hiyo baada ya kuonyesha kiwango bora kabisa katika mechi za mwezi huo, akifunga mabao mawili katika mechi mbili na kuisaidia Azam FC kuvuna pointi zote sita dhidi ya KMC (2-1) na Biashara United (2-0).

Aliwashinda wachezaji wenzake wawili ambao ni Erick mwijage wa Kagera Sugar na kipa namba moja wa Yanga, Metacha Mnata.

Mbali na Dube pia Lwandamina ametwaa tuzo ya kocha bora mwezi Mei ambapo aliwashinda Francis Baraza wa Kagera Sugar na Abdalah Mohamed wa JKT Tanzania.


KUMBE! MORRISON ALIZUIWA KUSHANGILIA NA WACHEZAJI PAMOJA NA KOCHA YANGA WATAJA NAMNA WATAKAVYORUDI KIMATAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply