Home Simba SC GOMES WA SIMBA AWEKA REKODI YAKE DAKIKA 360

GOMES WA SIMBA AWEKA REKODI YAKE DAKIKA 360


 DOZI ambayo kwa sasa Simba chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes kwa wapinzani wao inatoa wanapokutana uwanjani ni mwendo wa tatutatu katika mechi zao ikiwa ni rekodi ya kipekee kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Bongo.

Kazi ilianza Mei 22, Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya robo fainali, ubao ulisoma Simba 3-0 Kaizer Chiefs, ila licha ya ushindi huo ilitolewa kwa kuwa mchezo wa kwanza Uwanja wa FNB  Soccer City ubao ulisoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba.

Mei 26, mchezo wa Kombe la Shirikisho mbele ya Dodoma Jiji, ubao ulisoma Simba 3-1 Dodoma Jiji na ushindi huo uliwapa nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ambapo watakutana na Azam FC katika mchezo wa nusu fainali.

Mei 29, Uwanja wa Majaliwa, mchezo wa ligi walisepa na pointi tatu mazima na ubao ulisoma Namungo 1-3 Simba funga kazi ilikuwa juzi, Juni 3, Uwanja wa CCM Kirumba ambapo ubao ulisoma Ruvu Shooting 0-3 Simba.

Katika mechi nne ambazo ni dakika 360, Gomes ameshuhudia jumla ya mabao 12 wachezaji wake wakifunga na kipa wake namba moja Aishi Manula ameokota mabao mawili, kwenye msako wa pointi tisa wamesepa nazo zote wakiwa ni vinara katika ligi na pointi zao 64.

Gomes amesema kuwa kikubwa anachotazama ni ushindi kwenye mechi zao ambazo wanacheza ili kufikia malengo yao.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunashinda mechi zetu na kila kitu kinawezekana kwa kuwa wachezaji wanajiamini na wana uwezo mkubwa,” amesema.

 

SOMA NA HII  AL MERRIKH WALIA KUHUJUMIWA, WACHEZAJI NANE WAKUTWA NA CORONA