Simba SC

KAKOLANYA AJIFUNGA MIAKA MIWILI SIMBA

admin June 9, 2021 7:47 am


 IMEELEZWA kuwa kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya ameongeza dili la miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabosi wake hao.

Licha ya kwamba hana nafasi kikosi cha kwanza kwa kuwa namba moja ni Aishi Manula nyota huyo atakuwa hapo mpaka 2023.

Awali nyota huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye mpango wa kutolewa kwa mkopo kwenda Klabu ya Azam FC ila dili hilo lilibuma.

Kakolanya kwenye mechi za kimataifa msimu huu ambapo Simba iliishia hatua ya robo fainali alicheza mchezo mmoja kwenye hatua ya makundi.

Ilikuwa mbele ya Al Merrikh wakati huo Manula alikuwa anaumwa.

 


YANGA KAZI INAENDELEA, MATIZI KAMA KAWAIDA VIDEO: YANGA WATINGA FIFA KUDAI POINTI 3 ZA YANGA, MKUDE,AJIBU RUKSA KUJIUNGA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply