kimataifa

KIPA WA TIMU YA TAIFA YA ITALIA KUIBUKIA PSG

admin June 12, 2021 6:47 am


KIPA wa timu ya taifa ya Italia, Gianluigi Donnarumma yupo kwenye mpango wa kukamilisha masuala ya vipimo na Paris Saint Germain ya Ufaransa ambao wanapewa nafasi ya kupata saini yake akiwa ni mchezaji huru.

Kipa huyo mwenye miaka 22 alikuwa kwenye lango wakati timu ya taifa ya Italia ikishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Turkey kwenye mchezo wa Euro 2020 ndani ya Uwanja wa Olimpico. Kipa huyo alianza kuitumikia AC Milan akiwa na miaka 16.

Donnarumma ndani ya San Siro mkataba wake unameguka Juni 30 na inaelezwa kuwa AC Milan haina mpango wa kumuongezea dili jipya wanafikiria kumtumia Mike Maignan ambaye anatarajiwa kujiunga na AC Milan,Julai 2021 akitokea Klabu ya Lille.

Wakala wa mchezaji huyo ambaye ni Mino Raiola imeripotiwa kwamba amekubali uhamisho wa mchezaji huyo kwenda PSG wakiwa wamekubaliana katika baadhi ya mipango ambapo anaweza kufanya vipimo hivi karibuni.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI VIDEO: FLAVIANA MATATA AMUITA DIAMOND

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply