EURO 2020

YUPO JUU CRISTIANO RONALDO NAMBA MOJA KWA UTUPIAJI EURO

admin June 16, 2021 3:47 am

 CRISTIANO Ronaldo nyota wa timu ya Taifa ya Ureno amevunja rekodi ya Michel Platini wa Ufaransa ya kufunga mabao mengi ndani ya UEFA European Championship.

Ushindi walioupata usiku wa kuamkia leo baada ya ubao wa Uwanja wa Ferenc Puskas kusoma Hungray 0-3 Ureno kumemfanya Ronaldo kuwa mfungaji bora wa muda wote katika UEFA European Championship. 

Ni Raphael Guerreiro alianza kupachika bao la kwanza katika mchezo huo wa Euro 2020 kisha Ronaldo alipachika bao la pili dakika ya 87 kwa penalti na la tatu alipachika dakika ya 90+2 

Mabao hayo mawili yanamfanya Robaldo kufikisha jumla ya mabao 11 katika Euro akiwa amecheza jumla ya mechi 22 huku Platini wa Ufaransa rekodi yake ilikuwa ni mabao 9 katika mechi tano ambazo alicheza ma nafasi ya tatu ni ya Alan Shearer wa England ambaye alitupia mabao 7 katika mechi 9 alizocheza.

Tofauti ya Mreno na Mfaransa huyo ni kwamba Platini alipachika mabao yote hayo katika mashindano ya mwaka 1984 huku Ronaldo akifunga mabao hayo katika mashindano matano tofauti.

UFARANSA YAFUNGUA EURO 2020 KWA USHINDI, POGBA NYOTA WA MCHEZO YANGA YAINGIA ANGA ZA KIUNGO HUYU MCONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply