Ligi Kuu
FAINALI YA U 20 LEO, YANGA V MTIBWA SUGAR, AZAM V SIMBA
LEO Juni 19, Uwanja wa Azam Complex kutakuwa na mchezo wa fainali ya Ligi Kuu ya Vijana, U 20 ambapo ni Yanga v Mtibwa Sugar saa 1:00 usiku.
Yanga ilitinga hatua ya fainali baada ya ushindi wa penalti 6-5 mbele ya Azam FC baada ya dakika za kawaida ubao wa Azam Complex kusoma Azam 1-1 Yanga.
Mtibwa Sugar wao waliwanyoosha Simba mabao 3-1 katika mchezo wa nusu fainali.
Saa 10:00 ni mchezo wa kumtafuta mshindi wa pili kati ya Azam FC v Simba.

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.