Yanga SC

YANGA WARUDISHA SHUKRAN KWA MASHABIKI WAO

admin June 26, 2021 3:47 pm


 UONGOZI wa Yanga umerejesha shukrani kwa mashabiki wake ambao walijitokeza kwa wingi jana Juni 25, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United na mtupiaji akiwa ni Yacouba Songne.

Ushindi huo unafanya timu hiyo itinge hatua ya fainali ambapo sasa ni rasmi itakutana na Simba ambayo imecheza leo mbele ya Azam FC.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Kigoma na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa watani hao wa jadi.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa ni jambo la furaha kwa timu hiyo kutinga fainali hivyo mashabiki wanastahili pongezi.

VIDEO: MASHABIKI WAMFUATA DUBE SONGEA, ZOEZI LA PICHA LIKAFUATA SASA NI RASMI FAINALI ITAKUWA SIMBA V YANGA, KIGOMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply