Simba SC

SIMBA HESABU ZAO NI MBELE YA YANGA, KWA MKAPA

admin June 28, 2021 1:47 pm


 ERASTO Nyoni kiraka wa Simba amesema kuwa wanaamini kwamba watafanya vizuri kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Yanga kwenye Ligi Kuu Bara.

Nyoni alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichoweza kupata ushindi mbele ya Azam FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali, Songea ambapo ni nyumbani kwao pia.

Kiraka huyo ambaye aliibuka ndani ya Simba akitokea Azam FC ameweka wazi kwamba kwa sasa hesabu za timu hiyo ni kwenye mchezo wao ujao ambao ni dhidi ya Yanga.

“Kuhusu fainali yetu najua iyo ipo tu kwa namna yoyote hivyo mawazo yetu ni kuona kwamba mechi yetu ijayo ya ligi tunapata matokeo.

“Mashabiki waendelee kutupa sapoti na wale waliokuja Songea, kunyumba, ninawaambia kwamba asante sana kwa kuwa wamekuwa pamoja nasi kazi lazima iendelee,” amesema Nyoni. 

Mchezo wao unatarajiwa kuchezwa Julai 3, saa 11:00 jioni baada ya ule wa awali, Mei 8 kuyeyuka kutokana na mabadiliko ya muda yaliyofanywa ghafla na Bodi ya Ligi Tanzania jambo lililopelekea Yanga kugomea mabadiliko hayo ya muda.

MABOSI WA KARIAKOO WAINGIA KAZINI KUISAKA SAINI YA MAKUSU MUNDELE VIDEO: YANGA HAKUNA MAKANDOMAKANDO, SIMBA WAJE MUDA ULIOPANGWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply