Home Simba SC GOMES ATAKA KOMBE KWENYE MECHI DHIDI YA YANGA

GOMES ATAKA KOMBE KWENYE MECHI DHIDI YA YANGA


VINARA wa Ligi Kuu Bara, Simba tayari wako Mwanza kuikabili Polisi Tanzania, huku Kocha Mkuu wake, Didier Gomes akiweka bayana kwamba wanahitaji ushindi wa mechi zao tatu, lakini watafurahi kama mechi yao ya Yanga itawapa ndoo.

Simba inahitaji pointi 10 tu, kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo na Gomes alisema siku tatu zilizopita alifanya kikao na nyota wake kuwaeleza wanatakiwa kushinda mechi nne mfululizo kati ya saba walizonazo mkononi kufungia msimu.

Gomes alisema wanaanza kazi hiyo dhidi ya Polisi Tanzania leo kisha wanarudi Dar es Salaam kumalizana na Mbeya City kabla ya kuvaana na Yanga Julai 3 na kudai mechi hii ni muhimu kwao.

 “Tumedhamiria kuifunga Yanga, hii ni mechi muhimu yenye kuweka rekodi kubwa kwetu kwa kutangaza ubingwa katika mchezo mkubwa na naimani hilo linawezekana,” alisema Gomes.

Hesabu za Simba ni kwamba, kama itashinda mechi ya mechi tatu mfululizo za ligi ikiwemo ya Yanga, itafikisha pointi 76, ambazo haziwezi kufikiwa na watani wao hao waliopo nafasi ya pili kwa sasa na alama zao 61.

Yanga imesaliwa na mechi tano na kama itashinda zote ina uwezo wa kufikisha pointi 76.

AJIBU ATEMWA

Katika msafara wa Simba, Ibrahim Ajibu hayupo na hata katika mazoezi ya siku mbili hakuwepo. Mwanaspoti lilipomuuliza, Gomes alisema alipokea taarifa ya watabibu wa kikosi hicho ambao walimueleza kuwa Ajibu, anaumwa na amepewa muda kwa ajili ya matibabu zaidi.

Gomes alisema alirejea nchini Ijumaa kutokea Ufaransa kwa mapumziko mafupi na alipatiwa taarifa kuwa Ajibu anaumwa na anaendelea na matibabu.

“Ajibu amepata ruhusa ya matibabu,” alisema

SOMA NA HII  KWA TAARIFA YAKO...MAYELE NA KAGERE NI KITU KIMOJA...WOTE WAZEE WA KUTETEMA , WABAYA WA DK ZA JIONI...