Home Simba SC KIEMBA – MKUDE NA SIMBA SC , ‘NI SAWA NA MBWA...

KIEMBA – MKUDE NA SIMBA SC , ‘NI SAWA NA MBWA KUTAFUTIWA JINA BAYA’


WAKATI leo Jumatatu hukumu yake ikitarajiwa kutoka kutokana na kile kilichoelezwa kuwa utovu wa nidhamu, mchambuzi wa masuala ya michezo na nyota wa zamani wa Simba, Amri Kiemba amesema kuwa huenda mabosi hao wanamtafutia sababu.

Hii inakuwa ni mara ya pili ndani ya msimu wa 2020/21 kwa nyota huyo kusimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu ambapo zama za Sven Vandenbroeck alisimamishwa na kukosa jumla ya mechi 10.

Kwa sasa zama za Didier Gomes, pia amesimamishwa na mchezo wake wa mwisho kucheza ilikuwa dhidi ya Kaizer Chiefs nchini Afrika Kusini.

Kiemba amesema:”Tangu nacheza nae Mkude ni yule yule na hatukuwahi kusikia haya tunayosikia sasa wala hizi kesi tunazozisikia hivi sasa.

“Nahisi labda kwakuwa haitajiki tena ndani ya timu ndio maana haya tunasikia sana, yanatokea mengi ili siku akiondoka basi Mashabiki wasihoji sana, hii ni sawa na kumpa Mbwa jina baya ili umpige” .

SOMA NA HII  BAADA YA KUTOLEWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA....SIMBA SC WAAPA KUIHARIBIA YANGA SC...