Home Yanga SC KIKWETE ASIMULIA JINSI ALIVYOSHIRIKI ‘KULOGA’ ILIA YANGA ISHINDE

KIKWETE ASIMULIA JINSI ALIVYOSHIRIKI ‘KULOGA’ ILIA YANGA ISHINDE

Rais wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Kikwete aliwavunja mbavu wajumbe wa mkutano mkuu wa Yanga wakati akisimulia namna alivyoshiriki kwenye mambo ya kamati ya ufundi wakati akiwa kijana.

Amesema katika ujana wake amekuwepo kwenye mambo hayo Yanga.

JK ambaye alianza kwa kumuulizia Ramesh Patel kama yupo kwenye mkutano hao na kuambiwa ametangulia mbele za haki na kusikitika kisha kumuombea na kutoa stori yake wakati huo akiwa mweka hazina wa Yanga.

“Nilienda klabuni siku moja nikasikia wanalalamika watoto wacheza kavu kavu, hataki kutoa pesa, wakati kamati ya ufundi inataka ng’ombe.

“Nikaenda kwa Ramesh, tukasalimiana jambo jambo, nikamwambia kaka Ramesh rafiki yangu nina salamu zako” anasimulia

“Wanasema hutoi pesa kuipa kamati ya ufundi, vijana wanacheza kavu kavu, akanijibu ile ganga (mganga) ganga gani hovyo tu, Gombe (kombe) hawezi kunipa,” anasimulia Dk Kikwete akizungumza kwa lafudhi ya Ramesh

Amesema ambacho jamaa zake hao wa kamati ya ufundi hawakufahamu ni kwamba mweka hazina wao ni baniani, hawezi kutoa pesa wakanunue ng’ombe wa kuchinjwa kwenye mechi.

“Nilirudi nikawambia mweka hazina baniani, hivyo nendeni kwa Sharif, yule anachinja atawapa ng’ombe,” amesema Dk Kikwete huku akicheka lakini akasisitiza watu wasiamini kamati ya ufundi na badala yake wekeza kwenye mpira kwa kuwa na makocha na wachezaji wazuri.

SOMA NA HII  NABI: BADO TIMU HAIJAPATA MUUNGANIKO KWA SASA