Home news KUMBE! KAHATA ALIPATA TAARIFA JINA LAKE KUONDOLEWA KWENYE LIGI KATIKA MITANDAO

KUMBE! KAHATA ALIPATA TAARIFA JINA LAKE KUONDOLEWA KWENYE LIGI KATIKA MITANDAO


 KIUNGO wa zamani wa Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, Francis Kahata amesema kuwa ishu ya jina lake kuondolewa kwenye Ligi Kuu Bara alipata kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa sasa Kahata ni mchezaji huru baada ya mabosi wake wa Simba kugomea kumuongezea dili jipya kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Alijiunga na Simba akitokeoa Klabu ya Gor Mahia ambapo akiwa huko aliwahi kucheza na mshikaji wake Meddie Kagere ambaye naye kwa sasa mkataba wake ndani ya Simba unafika ukingoni.

Kahata alitolewa kwenye orodha ya wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu Bara baada ya Simba kumsajili Perfect Chikwende na jina lake likabaki kwenye orodha ya wachezaji watakaoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na timu hiyo ikaishia hatua ya robo fainali.

Kahata amesema:”Kuhusu jina langu kuondolewa kwenye kushiriki ligi nilipata taarifa hizo kwenye mtandao kwa sababu sikuwepo Tanzania ila niporudi nikakutana na taarifa hizo,” .

Mkataba wake ulipaswa kumeguka mazima Julai 4 ila kwa kuwa kwa sasa hana kazi ya kufanya ndani ya timu aliamua kuaga mazima hivyo yupo huru kujiunga na timu yoyote.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU