Home Simba SC MORRISON ANAAMINI KWAMBA YANGA WANATAKA KUMPOTEZA MAZIMA TANZANIA

MORRISON ANAAMINI KWAMBA YANGA WANATAKA KUMPOTEZA MAZIMA TANZANIA


BAADA ya Klabu ya Yanga kutoa taarifa 
kuwa Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Cas) imeanza kusikiliza pingamizi la awali la shauri la kimkataba la kiungo Bernard Morrison wa Simba, mchezaji huyo amefunguka mazito.

Akizungumza kwa hisia juu ya kile ambacho kinaendelea baina yake na Yanga, Morrison alisema anachofikiri kwa sasa ni kwamba viongozi wa Yanga wanataka kumpoteza mazima kwenye ardhi ya Tanzania.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Morrison alifafanua kuwa anachohisi kwenye moyo wake, Yanga hawataki arudi tena kwenye timu yao na hata mashabiki hawatamani tena kuona hilo likitokea, ila jambo pekee wanalotaka ni yeye kutocheza tena soka kwenye timu yoyote Tanzania.

“Nahisi viongozi wa Yanga hawataki kuona nikiendelea kuwepo Tanzania au nikicheza kwenye timu nyingine hapa. Nafikiri huo ndiyo mpango wao, kwa sababu sidhani kama wanahitaji nirudi tena kwenye timu yao.

“Maana hata mashabiki na wanachama sidhani kama wanahitaji kuona hilo likitokea. Siwezi kusema kuwa ni wivu au hawataki kuona nikiwa Simba, mawazo yangu yanaona kuwa wanataka niondoke kabisa hapa,” alisema Morrison.

Kwenye taarifa ya Yanga ilieleza kuwa Cas wangetoa majibu wa mwenendo wa kesi hiyo juzi Juni 2, jambo ambalo halikufanyika na hakuna taarifa yoyote kutoka ndani ya Yanga ambayo ilitolewa juu ya shauri hilo.

SOMA NA HII  CHAMA HAAMINI MACHO YAKE, UONGOZI WA SIMBA WAMFANYIA UMAFIA