Home Simba SC SAKATA LA MORRISON NA YANGA LINAANZA UPYA KABISA

SAKATA LA MORRISON NA YANGA LINAANZA UPYA KABISA

 


NYOTA wa Simba, Bernard Morrison sakata la mkataba wake limeanza upya kufukuta.

Kesi yake kuhusu utata wa usajili na Klabu ya Yanga katika Mahakama ya Usuluhishi wa Kimichezo, (Cas) inatarajiwa kuanza kusikilizwa leo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa Cas wamethibitisha kupokea barua ya rufaa ya kesi hiyo tangu Mei 25 mwaka huu.

“Pande zote mbili kwa maana ya klabu ba mchezaji tumetakiwa kupeleka maelezo Cas na hadi kufikia Juni 2 mwaka huu tayari kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

“Kama klabu sisi Yanga tutapeleka maelezo ila hatujajua kuhusu huyo mchezaji kikubwa tunataka kuona haki inatendeka,” .

Kwa sasa Morrison ambaye alisaini dili la miaka miwili Simba akitokea Yanga yupo zake Mwanza ambapo timu yake kesho ina mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting. 

Ishu yake ilisikilizwa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) ambao wao walieleza kuwa mkataba wake ulikuwa na mapungufu hasa kwa upande wa tarehe na baadhi ya karatasi kukutwa zimechwanwa na kumpa mamlaka nyota huyo kuwa huru.

Jambo hilo lilimfanya Yanga wakate rufaa kwa kuwa wanadai kwamba mteja wao alisaini dili la miaka miwili ila yeye anadai kwamba alisaini dili la miezi sita.

SOMA NA HII  SIMBA YATOA AHADI HII MECHI YA LEO AFL