Home news WALTER BWALYA AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUJA TANZANIA

WALTER BWALYA AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUJA TANZANIA


 LICHA ya kuwa kwenye mpango wa kuachwa 
kwenye kikosi cha Al Ahly kutokana na kushindwa kuonyesha kiwango, mshambuliaji wa timu hiyo, Walter Bwalya raia wa DR Congo amesema kuwa bado hajawa na mpango wa kujiunga na timu yoyote nchini, ikiwemo Simba.

Bwalya amejiunga na Al Ahly mapema mwaka huu kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu akitokea Al Gouna zote zikiwa za Misri lakini ameshindwa kuonyesha kiwango katika safu ya ushambuliaji wa timu hiyo inayonolewa na Pitso Mosimane raia wa Afrika Kusini ambaye alipendekeza usajili wa mshumbualiji huyo kabla ya kuibuka kwa suala la kutakiwa kuachwa.

Bwalya amesema kuwa mipango yake ni kuendelea kubakia kwenye timu hiyo na hana malengo yoyote ya kujiunga na klabu za Tanzania ikiwemo Simba.

“Nipo na timu ya taifa nyumbani, DR Congo, kuhusu suala na Simba au timu kutoka Tanzania, sijui chochote kwani mimi ni mchezaji wa Al Ahly na ndiyo sehemu ambayo yapo malengo yangu kwa sasa kuhakikisha timu inafanya vizuri.

“Lakini sijui kwa sasa kama nitaweza kucheza huko katika timu yoyote kwa sababu sijawa na mpango huo wala kufikiria maana nataka kuangalia malengo na mipango mingine katika sehemu ambayo nafanya kazi kwa sasa,” .


SOMA NA HII  SADIO KANOUTE 'AMBALAGAZA' MZAMIRU SIMBA...JAMBO LAKE LAENDA KAMA ALIVYOTAKA...