Home Yanga SC KUELEKEA KESHO, VIGOGO YANGA WAITANA CHEMBA CHAP NA KUJA NA HAYA

KUELEKEA KESHO, VIGOGO YANGA WAITANA CHEMBA CHAP NA KUJA NA HAYA


YANGA wanahesabu zao kuelekea mechi ya Simba na sasa ni kama mkutano mkuu ulirejesha umoja fulani mzito kwa vigogo wa timu hiyo na bilionea Ghalib Mohamed amewaita mezani watu wasiopungua 17.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga ni kwamba, Ghalib maarufu kama GSM amepania kuona Yanga inatoka salama amewaita vigogo wote wanaounda Kamati ya Mashindano ambayo ni kama imerudi.

Vigogo hao walioongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Hamad Islam na makamu wake, Hersi Said wamekutana na Ghalib kisha wakasuka mipango usiku na kila mmoja akaondoka na jukumu lake dhidi ya Simba.

Simba inakutana na Yanga katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Julai 3,2021 pale Uwanja wa Mkapa ambapo Simba wakiingia na akili ya kutafuta ushindi ili wachukue ubingwa wakati Yanga wakiwa hawana cha kupoteza, bali kutibua hesabu za mtani.

Kikao hicho habari mbaya kwa Simba ni kwamba ramani hiyo sio tu kwa ajili ya mchezo wa Julai 3 lakini pia vigogo hao wakiwemo pia wale wa zamani wa Yanga kina Samuel Lukumay, Said Ntimizi, Deo Mutta, Hussein Nyika na wengine pia wanachora ramani ya mchezo wa fainali ya FA baina ya timu hizo.

“Sisi huku kama viongozi tayari tumeshaungana na wanachama nao kila mmoja anatakiwa kuipigania timu kwa nafasi yake, hatutarajii kuona wanachama nao wakiiacha timu peke yao nao wapambane na siku ya mchezo pia waje kwa wingi,” kilisema chanzo chetu ndani ya uongozi.

Hatua hiyo inaweza ikawa mzuka mkubwa ndani ya Yanga na kutokana na kamati hiyo Mwanaspoti linafahamu kwamba haikuwa pamoja kwa muda mrefu wakibaki wajumbe wachache tu huku kila mmoja alikuwa akiipigania timu hiyo kivyake.

NINJA MZUKA MWINGI

Wakati vigogo hao wakiungana, habari njema katika timu yao ikawa kurejea kwa beki mbishi Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na sasa ameshtua na kuleta changamoto mpya ya nani anaweza kupangwa katika safu ya ulinzi katika mchezo huo.

Ninja amerejea sambamba na beki mwingine, Mustapha Yassin, lakini taarifa kutoka ndani ya kikosi hicho ni kwamba Ninja pekee ndiye ameonekana kuwa katika sura ya kuweza kuvaa jezi katika mchezo huo.

SOMA NA HII  MRITHI WA MAYELE YANGA HALI TETE AKOSA PAKUSHIKA

Hata hivyo, uamuzi wa beki huyo kucheza utabaki kwa kocha Nesreddine Nabi ambaye tayari uhakika amewaweka kando mastaa watatu wa kigeni – kiungo Haruna Niyonzima, beki na nahodha mkuu Lamine Moro na mshambuliaji Michael Sarpong, huku akiwaambia mabosi wake kwamba kwa wachezaji waliobaki bado anaweza kushinda mbele ya Simba.