Ligi Kuu

IHEFU KUIVAA YANGA KWA TAHADHARI

admin July 15, 2021 4:47 am
KOCHA Mkuu wa Ihefu yenye maskani yake Mbeya, Zuberi Katwila amesema kuwawataingia kwenye mchezo wa leo dhidi ya Yanga kwa tahadhari kubwa ili waweze kushinda.

 

Ihefu inatarajia kukutana na Yanga leo Julai 15, Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya kutafuta pointi tatu zitakazowasaidia kujiweka sehemu nzuri ya kuepuka kushuka daraja.

 

Katwila amesema kuwa, mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa upande wao ili kujihakikishia usalama wa kubaki ligi kuu msimu ujao.

 

“Tumekuja kwa tahadhari ya hali ya juu kwa sababu tunaenda kucheza na timu kubwa na yenye uwezo mkubwa pia kwa hiyo tupo makini sana katika mchezo huu na tumejipanga vizuri.

 

“Wachezaji wote wapo salama kabisa na wote kwa pamoja tumekuja kutafuta pointi tatu zitakazotusaidia kuepuka na hatari ya kushuka daraja,” amesema Katwila.


Ihefu hadi sasa imekusanya pointi 35 katika michezo 32 iliyocheza ya ligi Kuu Bara na kupata ushindi katika michezo tisa, wamepoteza 15 na kutoa sare 8.

MSIMAMO WA LIGI KUU BARA UPO NAMNA HII KWA SASA MUONEKANO WA NDINGA MPYA YA YANGA BAADA YA KUFANYIWA MABORESHO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply