Yanga SC

YANGA WARUDISHA SHUKRAN KWA MASHABIKI

admin July 26, 2021 11:43 am

 UONGOZI wa Yanga umewashukuru mashabiki wao ambao walijitokeza kwa wingi jana kuipa sapoti timu hiyo.

Ni katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika,  Kigoma mwisho wa reli. 

Licha ya jitihada za wachezaji kusaka ushindi ngoma ilikuwa nzito kwa Yanga kwa kuwa walikubali kuokota bao moja nyavuni. 

Ilikuwa kupitia kiungo mkabaji, Taddeo Lwanga aliyepachika bao hilo kwa bichwa dakika ya 76 na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. 

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Yanga wameandika kwamba shukrani kwa mashabiki waliojitokeza kuipa sapoti timu ya Wananchi.

Tayari kikosi kimerejea Dar es Salaam wakiwa na medali za mshindi wa pili na taji limeelekea kwa watani zao Simba ambao nao waharejea Dar.

MABINGWA WA KOMBE LA SHIRIKISHO WATIA TIMU DAR NA TAJI LAO SIMBA WATAJA SABABU YA KUTOSHIRIKI KAGAME CUP , YANGA WATAJWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply