kimataifa

TAMMY ABRAHAM BEI YAKE YASHUSHWA

admin August 1, 2021 12:43 pm


 IMERIPOTIWA kwamba bei ya nyota wa Chelsea Tammy Abraham imeshushwa ili aweze kuuzwa kwa timu ambayo inamuhitaji ambapo Arsenal inapewa nafasi kubwa ya kumpata mshambuiaji huyo kwa dau ambalo linaweza kuwa chini ya pauni milioni 40.

Awali mabosi wa Chelsea walikuwa wanahitaji kupewa pauni milioni 40 kwa ajili ya kumuuza mchezaji huyo ila mambo yamekuwa tofauti sokoni kwa kuwa anaonekana kudoda.

Abraham mwenye miaka 23 hajawa na nafasi kikosi cha kwanza baada ya timu hiyo ya Chelsea kuchukuliwa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel ambaye alishinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ni pauni milioni tano ambazo inaripotiwa kwamba Chelsea inayotumia Uwanja wa Stamford Bridge kwenye mechi zake za nyumbani inapanga kuzikata jumla ili aweze kuibukia ndani ya Uwanja wa Emirates msimu ujao.

Mikel Arteta Kocha Mkuu wa Arsenal inaelezwa kuwa amekuwa njia panda ili aweze kumsajili mchezaji huyo kwa kuwa wanaona kwamba gharama iliyopunguzwa ni kubwa mpaka kufikisha dau la pauni milioni 35.

VIDEO: KOCHA KIM POULSEN ACHEZA SINGELI, KISA UBINGWA WA CECAFA VIDEO: BASHUNGWA AKABIDHIWA KOMBE LA CECAFA LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply