Simba SC

KUMBE KAIZER CHIEF WALIMTAKA LUIS KWA PESA NYINGI ZAIDI YA DAU LA AL AHLY

admin August 4, 2021 5:00 pm


KAIZER Chiefs waliongeza dau kwa mzigo Simba, ili kumpata  Luis Miqussone aliyeko kwenye hatua za mwisho kutimkia Al Ahly.

Habari za uhakika ambazo gazeti la Mwanaspoti imezipata ndani ya Simba ni kwamba, Kaizer Chiefs walionyesha nia ya kuweka mezani Sh 1.5 Bil ikiwa imezidi ile Bil 1 ya Al Ahly ya Misri.

Lakini gazeti la Mwanaspoti linajua kwamba Luis amewaambia marafiki zake wa karibu ndani ya Simba kwamba anakwenda Al Ahly.

Hadi jana Uongozi wa Ahly ulikamilisha rasmi uhamisho wa winga huyo kutoka Simba kwa ada ya Dola 900,000

Usajili wa winga huyo umekamilika  baada ya kufikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo

Mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Afrika mara 10 walifikia makubaliano na Simba tangu wiki iliyopita na kilichobakia ilikuwa ni kumalizana na mchezaji huyo.

KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA ALTABARA KAGAME CUP PETER BANDA ANA TUZO YA UFUNGAJI BORA, APITA NYAYO ZA BABA YAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply