Home Yanga SC HASIRA ZA KUMKOSA HENOCK ZAWAFANYA YANGA KUKIMBILIA KIFAA HATARI CHA SVEN

HASIRA ZA KUMKOSA HENOCK ZAWAFANYA YANGA KUKIMBILIA KIFAA HATARI CHA SVEN


BAADA ya beki Mkongomani, Henock Inonga kuingia tamaa na kusaini Simba, Yanga wamebadili gia haraka na kutua kwa kifaa kingine.

Ni beki mahiri wa DR Congo, Yanick Bangala Litombo anayekipiga kwenye klabu ya FAR Rabat ya Morocco iliyoko chini ya kocha wa zamani wa Simba, Mbelgiji Sven Vandebroeck.

Habari za uhakika ambazo soka la bongo imezipata ni kwamba Yanga walikuwa wameweka uhakika mkubwa kwa Inonga wa DC Motema Pembe lakini baada ya kukumbana na sapraizi hiyo iliyofanywa na meneja wa mchezaji huyo, Senzo Mbata akawaambia Yanga tulieni.

Habari zinasema kwamba Senzo alicheki na wakala wa Bangala ambaye alikuja na Fiston Mayele kusaini Yanga Jijini Dar es Salaam na akamhakikishia kwamba wasiwe na presha kwani mchezaji huyo anammudu na anahitaji kuweka sawa mambo machache na FAR Rabat.

Habari zinasema kwamba jana walipambana na ishu hiyo kwa kiasi kikubwa imekaa vizuri kwani walishapatiwa gharama zake huku ikielezwa kwamba staa huyo hafurahii maisha Morocco na amemwambia meneja wake kwamba mambo yakikaa sawa atakuja Dar es Salaam.

Ingawa baadhi ya vigogo wa Yanga wanahoji baadhi ya vitendo vya utovu wa nidhamu vya Bangala, lakini Sven amepata taarifa zake za kutakiwa na Yanga na akashtuka lakini baadae akapuuzia.

Habari zinasema kwamba Meneja wa Bangala amewahakikishia kwamba wanaweza kumpata mchezaji huyo hata kwa mkopo na  wameshakamilisha ishu na mchezaji huyo awasubiri waungane naye kambini Morocco.

Yanga imepania kusuka upya safu yao ya ulinzi kwa kumpa beki mmoja mzoefu mwenye umbo kubwa kuziba nafasi ya Lamine Moro waliyempiga chini kwa sababu za kinidhamu. Mwanaspoti linafahamu pia kwamba kuna wakala mmoja wa Zimbabwe amewaletea Yanga mabeki wawili lakini hawajawatilia maanani kwani akili yao ipo kwa Bangala.

KIPA KUWAHI

Kipa bora wa ligi ya Mali, Diarra Djigui anatarajiwa kuwahi Jijini Dar es Salaam kufikia Jumatatu mchana tayari kujiunga na wenzie kujiaandaa na kambi ya kujifua nchini Morocco.

Djigui anakuja kuchukua nafasi ya kipa Mkenya, Farouk Shikalo ambaye hakuwa na msimu mzuri Jangwani.

SOMA NA HII  'BEKI LA CHAN' NA YANGA NI SUALA LA MUDA TU....MWENYEWE AANIKA A-Z ISHU ILIVYOPIGWA..

Habari zinasema kwamba wakala wa mchezaji huyo tayari ameshamalizana na Yanga na wameshamtumia tiketi ya kuja wiki ijayo.