Yanga SC

YANGA YAINGIA ANGA ZA KIPA HUYU WA MALI

admin August 7, 2021 3:43 am

 IMEELEZWA kuwa Yanga ipo kwenye hesabu za kumalizana na kipa namba moja wa timu ya taifa ya Mali ili aweze kujiunga na timu hiyo msimu wa 2021/22.

Nyota huyo kutoka Mali, anaitwa Diarra Djigui ana umri wa miaka 26, na ni nahodha wa timu ya taifa ya Mali iliyoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanaocheza kwenye ardhi ya nyumbani (CHAN) 2020.

Sababu kubwa ya Yanga kumuhitaji kipa huyo ni kuwa chaguo namba moja la kocha wa Yanga, Mtunisia Nesreddine Nabi ambaye amekuwa akitafuta kipa anayemtaka.

Kwa sasa Yanga ipo kwenye mpango wa kuboresha kikosi kwa kuwa wanashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika pia wanahitaji taji la ligi.

Ikiwa usajili wa nahodha huyo wa Mali utakamilika basi ni Faroukh Shikalo anaweza chimba kwa kuwa dili lake limeisha na bado hajasaini dili jipya.

SIMBA YATUMIA MBINU ZA YANGA KUMNASA STRAIKA, NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI CLATOUS CHAMA AFUNGUKA ISHU YA TUZO BONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply