Yanga SC

BREAKING: YANGA YAMSAJILI KIPA KUTOKA TIMU YA TAIFA YA MALI

admin August 8, 2021 9:43 am


 RASMI hesabu za kumsajili kipa namba moja wa timu ya taifa ya Mali zimekamilika na atakuwa na timu hiyo msimu wa 2021/22.

Nyota huyo kutoka Mali, anaitwa Diarra Djigui ana umri wa miaka 26, na ni nahodha wa timu ya taifa ya Mali iliyoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanaocheza kwenye ardhi ya nyumbani (CHAN) 2020.

Sababu kubwa ya Yanga kumpa dili kipa huyo ni kuwa chaguo namba moja la kocha wa Yanga, Mtunisia Nesreddine Nabi ambaye amekuwa akitafuta kipa anayemtaka.

Kwa sasa Yanga ipo kwenye mpango wa kuboresha kikosi kwa kuwa wanashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika pia wanahitaji taji la ligi.

Usajili wa nahodha huyo wa timu ya taifa ya Mali unatoa nafasi kwa Faroukh Shikalo kuchimba mazima Yanga.

Nyota huyo amepewa dili la miaka miwili kuitumikia timu hiyo.


YANGA:KILA MTU ANACHEZA KWA KIWANGO AMBACHO ANACHO BAADA YA KUTEMANA NA YANGA, CARLINHOS HUYU HAPA NA TIMU YAKE MPYA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply