Simba SC

MUGALU AINGIA ANGA ZA RS BERKANE YA MOROCCO

admin August 9, 2021 9:43 am


 IMEELEZWA kuwa mshambuliaji wa Simba, Chris Mugalu yupo kwenye rada za Klabu ya RS Berkane ya Morocco ambayo inafundishwa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge.

Ibenge anamtambua Mugalu kwa kuwa alikutana naye kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wakati ule anaifundisha AS Vita ya Congo.

Kwenye mchezo wa hatua ya makundi walipokutana Congo, Mugalu aliyeyusha furaha ya AS Vita kwa kufunga bao kwa penalti na aliwasumbua mabeki wa timu hiyo jambo ambalo limemfanya akubali uwezo wake.

 Ikiwa mambo yatakwenda sawa huenda dili hilo likamiliziwa nchini Morocco kwa kuwa Klabu ya Simba imepanga kwenda huko kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.

IMEISHA HIYO…YANGA WAMALIZANA CHAP NA KIUNGO HUYU WA SIMBA.. HUYU NDIYO MO ..BAADA YA PETER BANDA.. HIKI HAPA KIFAA KIPYAA KUTOKA MALI KUTUA MSIMBAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply