news

BIASHARA UNITED YAMALIZA BIASHARA NA MAJEMBE YA KAZI

admin August 11, 2021 6:43 am


 BIASHARA United wanaopenda kujiita Wanajeshi wa Mpakani wameanza kazi ya kutambulisha majembe mapya kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22.

Timu hiyo iliwatema nyota wake 17 ambao walikuwa nao msimu uliopita na kuwatakia kila la kheri itashiriki mashindano ya kimataifa katika Kombe la Shirikisho.

 Miongoni mwa nyota ambao wametambulishwa ni pamoja na Kassim Mdoe kutoka Tanzania Prisons  ametua mikononi mwa ‘Wanajeshi wa Mpakani’, Biashara United kwa dili la miaka miwili.

Jana Agosti 10 ilimtambulisha Aniseth Revocatus kutoka Mwadui FC, Toyo Odongo Matthew kutoka Zoo United ya Kenya.


Agosti 9 ilimtambulisha nyota Atupele Green Jakscon.Kwa mujibu wa uongozi wa Biashara United umeweka wazi kwamba usajili umekamilika kilichobaki ni muda wa kuwatambulisha wachezaji wao.
KMKM WAFUNGASHIWA VIRAGO KAGAME CUP AZAM FC KAZINI LEO KAGAME CUP, AZAM COMPLEX

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply