Home news KWISHA KAZI…WAMOROCCO WAFANYA KUFURU DAU LA KUMNG’OA CHAMA..SIMBA WAKUBALI KIAINA

KWISHA KAZI…WAMOROCCO WAFANYA KUFURU DAU LA KUMNG’OA CHAMA..SIMBA WAKUBALI KIAINA


MAFUNDI wawili wa mpira waliokuwa na chachandu za aina yake kwenye mechi ya watani wa jadi wameng’oka. Gazeti la  Mwanaspoti linameripoti kujua kwamba Yanga iko kwenye hatua za mwisho za kumuuza winga wao matata, Tuisila Kisinda nchini Morocco.

Simba nao wamepokea ofa ndefu kutoka na FR Rabat ya hukohuko Morocco kwaajili ya kumnunua staa wao mpaka rangi uwanjani, Clatous Chama.

Chama bado yupo Dar, lakini jana mchana Kisinda yeye alitua nchini humo akitokea kwao DR Congo kukamilisha uhamisho wa kuhamia klabu ya RS Berkane iliyoweka dola 300,000 mezani (Sh693milioni). Hilo ni dili kubwa kuwahi kufanywa na Yanga kwenye miaka ya hivi karibuni kwani Simon Msuva aliuzwa Difaa El Jadida ya Morroco kwa dola 80,000 (Sh184 milioni) huku Heritier Makambo akiuzwa Horoya ya Guinea kwa Euro 70,000 (Sh190 milioni).

Berkane imeweka kiwango kizuri cha fedha ambacho ni mara tatu na chenchi inabaki ukilinganisha na kiwango ambacho Yanga walichomnunulia awali. Kwa lugha rahisi ni kwamba mauzo ya Kisinda yamerudisha pesa na faida kubwa ya manunuzi yake na kiungo Mukoko Tonombe ambaye amemuacha Jangwani.

Yanga ilitumia dola 100,000 (Sh231 milioni) kuwanunua Kisinda na Mukoko mwaka mmoja uliopita ambapo winga huyo akitokea Union Maniema huku Mukoko akitokea AS Vita.

Hata hivyo, katika ada hiyo ya Yanga ambayo watalipwa na Berkane gazeti la  Mwanaspoti  limeripoti kuwa linafahamu kwamba klabu ya Maniema itajipatia asilimia 30 ya fedha hizo kulingana na makubaliano ya kimkataba wakati wanamnunua winga huyo.

Kisinda mwenyewe katika dili hilo atajichukulia kiasi cha dola 150,000 (Sh346 milioni) ikiwa ni kama mara tatu ya fedha ambazo alivuna akiingia Yanga.

Winga huyo sasa anakwenda kuungana na kocha wake wa zamani Florent Ibenge ambaye alifanya naye kazi AS Vita. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga injinia Hersi Said jana alithibitisha kutakiwa kwa Tuisila lakini akasema hata Yacouba Sogne na Mukoko Tonombe nao wana ofa zao mezani wanazijadili.

SOMA NA HII  KISA KUVAA SANA JEZI NYEUSI....YANGA WAFUNGULIWA KESI...

CHAMA MKWANJA MREFU

Wakati kiungo wa Simba, Clatous Chama akikanusha taarifa za kuuzwa kwake kwenda FAR Rabat ya Morocco, Mwanaspoti linajua kuna ofa ya dola 600,000 (Sh1.3 bilioni) iko mezani kwa Simba.

Chama alidai; “Hizo taarifa nimeziona kwenye Instagram kaka, bado nina mkataba wa miaka miwili na sijaambiwa lolote.” Lakini gazeti la  Mwanaspoti linadai kuwa linajua jana hakujumuishwa kwenye orodha ya wachezaji wa Simba wanaojiandaa kwenda kambini.

Wakati huo huo, wiki moja nyuma mchezaji huyo alikaririwa kupitia ukurasa wake wa Instagram alipokuwa mubashara (Live) akisema yupo tayari kuondoka kwenda timu yoyote kama tu mabosi wa Simba watakubaliana na timu hiyo.

Mmoja wa mabosi kutoka Simba alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti kuwa; “Bado hatujaafikiana moja kwa moja ila ofa imefika kwetu tayari na kama tukikubaliana basi atakwenda,” alisema kiongozi huyo.

Usajili wa Chama kwenye kikosi hicho ni kutokana na mapendekezo ya kocha wa FAR Rabat, Sven Vandenbroeck ambaye aliwahi kufanya kazi na mchezaji huyo akiwa Simba na kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu.

Kama Chama ataondoka katika klabu hiyo basi Simba watakuwa wamefanya biashara ya kuuza ya wachezaji wawili baada ya awali kumuuza Miquissone kwenda Al Ahly ya Misri kwa Sh2 bilioni ambao ni mkwanja mrefu kuwahi kufanyika kwenye soka la Tanzania.

Credit: Mwanaspoti