Yanga SC

WAKATI KISINDA AKISEPA .., YANGA WAAMUA KUSHUSHA KIBERENGE HIKI KINGINE HATARI ZAIDI YAKE

admin August 11, 2021 1:00 pm


KUNA mashine nyingine ambayo punde itatua kwenye ardhi ya Tanzania kama mambo yakienda kama yalivyopangwa.

Yanga imemalizana na winga Mkongomani, Ducapel Moloko ambaye ni mbadala wa Tuisila Kisinda ambaye muda wowote kuanzia sasa atasaini mkataba na Berkane ya Morocco.

Soka la Bongo limejihakikishia kwamba Moloko ameshafanya mazungumzo na Yanga na amewaambia wampe wiki moja tu aweke ishu zake sawa ajiunge nao kambini.

Yanga wanambeba Moloko ambaye amekuwa na uwezo mkubwa wa kusukuma mashambulizi na kufunga msimu huu. Mmoja wa viongozi wa Yanga alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti jana kwamba dili hilo litakuwa sapraizi kwa mashabiki na wanaamini kwamba mchezaji huyo ni sahihi kwa aina ya uchezaji wa Kisinda na matakwa ya Kocha Mohammed Nabi.

Moloko ndiye aliyeziba pengo ya Kisinda alipoondoka AS Vita na habari zinasema kwamba Mukoko Tonombe amehusika kumpendekeza. Habari zinasema kwamba Moloko anaweza kujiunga na timu hiyo dakika za mwisho jijini Dar es Salaam kabla ya kukwea pipa kwenda kambini Morocco au akichelewa ataunganisha juu kwa juu.

WAZIR JUNIOR APIGIA HESABU KUWA MFUNGAJI BORA BANDA AINGIA ANGA ZA WANAOLIPWA MKWANJA MREFU BONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply