WINGA wa Yanga, Dickson Ambundo amewashusha presha mashabiki kwa kuwaambia kuwa kila kitu kitakuwa sawa kwa msimu ujao wa 2021/22.
Nyota huyo ambaye ni ingizo jipya kutoka Dodoma Jiji, jana Agosti 11 alitambulishwa rasmi kwa kusaini dili la miaka miwili.
Alikuwa katika kikosi cha kwanza ambacho kilishiriki Kagame Cup Challenge 2021 na kuishia hatua ya makundi.
Katika mechi tatu ambazo alicheza alitoa pasi moja ya bao lilifungwa na mshikaji wake Wazir Junior.
Ambundo:”Bado Yanga wanapaswa watulie kuna mambo mengi mazuri yanakuja. Kushindwa kutwaa taji la Kagame sio mwisho wa mapambano,”.