Home Yanga SC BREAKING: YANGA YATAMBULISHA MAJEMBE MAWILI, YUPO MRITHI WA KISINDA

BREAKING: YANGA YATAMBULISHA MAJEMBE MAWILI, YUPO MRITHI WA KISINDA



UONGOZI wa Yanga leo Agosti 13 umewatambulisha nyota wao wawili ambao watakuwa ndani ya kikoi hicho kwa msimu wa 2021/22.


Djuma ni beki ambaye anapewa nafasi ya kufanya vizuri msimu ujao kwa kuwa uzoefu wake unambeba na amecheza timu kubwa ya AS Vita ya Congo. 

Ni Shaban Djuma ingizo jipya kutoka AS Vita pamoja na Jesus Moloko.

Moloko anakuwa mbadala wa Tuisila Kisinda ambaye anakwenda kujiunga na Klabu ya RS Berkane ya Morocco.

Moloko amebainisha kuwa hajawahi kufeli katika kazi ambazo huwa anafanya hivyo anaamini kwamba atafanya vizuri ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.


SOMA NA HII  WAKATI TETESI ZIKISEMA ONYANGO ATATUA YANGA....MANARA AIBUKA NA KUMKATAA MCHANA KWEUPEE..