KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu,Nasreddine Nabi leo Agosti 15 kimeanza safari ya kuelekea nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22.
Kitatua kwanza Dubai kisha kesho kitaunganisha safari mpaka Morocco ambapo tayari watani zao wa jadi Simba wameweka pia kambi..
Ni Nabi ambaye hayupo Bongo yeye ataunganisha moja kwa moja nchinj Morocco kuendelea na majukumu yake ya kazi.
Beki Juma Makapu baada ya dili lake kuisha anajiunga na Klabu Polisi Tanzania ambayo ataitumikia msimu ujao hivyo hayupo kwenye msafara wa leo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli kambi hiyo itadumu mpaka Septemba 26 na timu itarejea Tanzania, Septemba 27 kwa ajili ya maandalizi ya wiki ya Mwananchi.