Home Simba SC KUHUSU USIRI WA PESA ZA MAUZO YA CHAMA NA LUIS…., UFAFANUZI WA...

KUHUSU USIRI WA PESA ZA MAUZO YA CHAMA NA LUIS…., UFAFANUZI WA KINA HUU HAPA


KAIMU Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano ya Simba, Ezekiel Kamwaga ametolea ufafanuzi kwa watu wanaohoji taarifa ya timu hiyo kutoweka wazi gharama za mauzo na timu wanazokwenda wachezaji wake wawili Clatous Chama na Luis Miquissone.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Kamwaga alisema kuwa sio lazima klabu kutaja gharama iliyotumika kuuza au kununua mchezaji kwani katika ligi zilizoendelea duniani bei huwa hazitajwi akitolea mfano wakati Marouane Fellaini anatoka Everton kwenda Manchester United, bei haikutajwa.

“Iko hivi, kuna sababu za kusababisha gharama kutajwa na kuna sababu za kusababisha gharama zisitajwe Ni kawaida kabisa kwenye mpira, mfano mdogo wa kwanini wakati mwingine gharama hazitajwi,”Mchezaji anaweza kusajiliwa kwa dau kubwa sana na likawa mzigo kwake Washabiki wakategemea makubwa kwake mapema,” alisema.

“Kumsaidia asiwe na presha tangu mwanzo gharama zinafichwa Wakati mwingine timu inakuwa imelipa hela nyingi kiasi kwamba washabiki wake wanaweza kuhoji hela zote hizo mnampa huyu? Mbona yule mlimsajili kwa fedha kidogo? Timu inaamua kukaa kimya Sababu za kutotaja zipo nyingi sana,” alisema Kamwaga.

Kuhusu taarifa ya Simba kutotaja timu ambazo wachezaji hao wanaenda Kamwaga alisema Si lazima pia kwani Kila timu ina utaratibu wake wa kutangaza wachezaji wapya Wanataka wawe wa kwanza kutangaza mchezaji mpya na wanafaidika na hilo.

“Wanachotaka wewe wauzie mchezaji na wao watatangaza wenyewe mnakubaliana hivyo sasa katika mazingira hayo Simba SC haiwezi kusema wanaenda wapi kwa sababu itakiuka makubaliano,” amesema Kamwaga na kuongeza kuwa

“Muda si mrefu itajulikana wanaenda wapi na ungekuwa mkanganyiko zaidi kwenye taarifa moja tungesema huyu anaenda kule na huyu hatusemi, taarifa imeondoa huo mkanganyiko,”

SOMA NA HII  UKWELI MCHUNGU.....SIMBA ISIBEZWE KWA NUSU FAINAL YA YANGA CAF...