Home Simba SC SIMBA V YANGA SEPTEMBA 25, HAKUNA NAMNA, TIMU ZOTE KAMILI GADO

SIMBA V YANGA SEPTEMBA 25, HAKUNA NAMNA, TIMU ZOTE KAMILI GADO


 HAKUNA kisingizio Septemba 25, mwaka huu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utakuwa ni ufunguo wa msimu wa 2021/22 hapa nchini ambapo Simba SC watacheza dhidi ya Yanga SC.


Utamu wa mchezo huo 
utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, unazidi kuongezeka kutokana na timu zote kuonekekana kuimarika zaidi kutokana na usajili ambao umefanywa hadi sasa.

 

Msimu uliopita, Yanga waliteswa sana eneo la ushambuliaji ndiyo maana kwenye dirisha hili la usajili wamecheza zaidi kwenye eneo hilo kwa kusajili nyota ambao wanaamini wataleta mabadiliko.

 

Kwa usajili wa timu zote ambao umefanyika hadi sasa, Yanga wanaonekana kuimarika zaidi kwenye eneo la mbele wakiwa na maingizo mapya, Fiston Mayele, Heritier Makambo, Jesus Moloko na Dickson Ambundo.Nyota hao wanakwenda kuungana na nyota kama Deus Kaseke, Ditram Nchimbi na Yacouba Songne.


Wakati Yanga wakitamba na washambuliaji zaidi, Simba wao hawakuwa na shida sana kwenye eneo hilo baada ya kuwepo nyota kama John Bocco, Chris Mugalu na Meddie Kagere.

 

Wao wakaamua kucheza na viungo, wakimleta Peter Banda, Duncan Nyoni, Pape Ousmane Sakho, Abdulswamad Kassim na Sadio Kanoute ambao wanakwenda kuungana na Tadeo Lwanga, Jonas Mkude, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga na Rally Bwalya.

 

Ukiachana na timu zote kutamba na usajili wao huo, imebainika vikosi vyao vimekuwa vipana zaidi.

 

Kwa upande wa Yanga, kikosi chao cha kwanza chini ya Kocha Nadreddine Nabi, kinatarajiwa kuwa hivi; Diarra Djigui, Djuma Shabani, David Bryson, Bangala Litombo, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Feisal Salum, Khalid Aucho, Heriter Makambo, Fiston Mayele na Yacouba Songne.



Kikosi cha pili cha Yanga kinatarajiwa kuwa na nyota hawa, Erick Johora, Kibwana Shomari, Yasin Mustapha, Abdallah Shaibu, Dickson Job, Zawadi Mauya, Ducapel Moloko, Deus Kaseke, Yusuph Athumani, Saidi Ntibazonkiza na Dickson Ambundo.

 

Wakati vikosi hivyo viwili vikikamilika, nyota wengine watakuwa wakisubiri ambao ni Ramadhani Kabwili, Adeyum Salehe, Balama Mapinduzi, Paul Godfrey, Farid Mussa na Ditram Nchimbi.

SOMA NA HII  ACHANA NA YANGA KUWA BINGWA MSIMU HUU...MSHERY NAYE KAWEKA REKODI HII YA KIPEKEE JANGWANI....

 

Kwa upande wa Simba, kikosi chao cha kwanza kinatarajiwa kuwa hivi; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Henock Baka, Joash Onyango, Taddeo Lwanga, Peter Banda, Rally Bwalya, Chris Mugalu, John Bocco na Pape Ousmane Sakho.

 

Kikosi cha pili cha Simba kinatarajiwa kuwa hivi; Beno Kakolanya, Israel Mwenda, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Bernard Morrison, Sadio Kanoute, Meddie Kagere, Yusuph Mhilu na Duncan
Nyoni.

 

Wanaobaki ni Perfect Chikwende, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Abdulswamad Kassim, Mzamiru Yassin, Ibrahim Ame, sambamba na Jeremia Kisubi na Kibu Denis ambao wanatajwa kila mmoja kusaini mkataba wa miaka miwili ingawa bado hawajatangazwa rasmi.