Home Yanga SC NYOTA WA YANGA WALIOBAKI MOROCCO KUREJEA BONGO

NYOTA WA YANGA WALIOBAKI MOROCCO KUREJEA BONGO


NYOTA wa Yanga ambao walibaki nchini Morocco wanatarajiwa kurejea Tanzania kesho ili kuungana na timu katika maandalizi ya msimu wa 2021/21.

Sababu ya nyota hao kukwamwa inatajwa kuwa ni kushindwa kukamilisha suala vibali.

Nyota hao walibaki huko baada ya kambi kuvunjwa kutokana na sababu ambazo Yanga walieleza kuwa ni kwa maslahi mapana ya klabu.

Wapo wachezaji ambao walitangulia na wanaendelea na mazoezi katika kambi ya Avic iliyopo Kigamboni.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Yanga zimeeleza kuwa wachezaji hao walikuwa wanaendelea na mazoezi hivyo wapo imara.

Ni Yacouba Songne,  Dickson Ambundo, Djuma Shaba, Fiston Mayele pamoja na wengine ambao wanatarajiwa kurejea kesho ili kuungana na timu kuelekea Wiki ya Mwananchi.

SOMA NA HII  MANARA AFUNGUKA KUHUSU MO DEWJI NA AINA YA WATU ANAOWAPENDA